Seventh-Day Adventist Church

Kimara Sda Church Offical Website

Menu

Historia ya kanisa la Kimara SDA

Add a Slideshow to see your custom images here

HISTORIA YA KANISA LA KIMARA –(23 Nov, 2014)

UTANGULIZI

Tunamshukuru Mungu kutuweka hai na kutuwezesha kufikia hatua hii,Jina la Bwana lipewe sifa.

 

MAHALI KANISA LILIPO

Kanisa la Kimara lipo eneo la Kimara Resort kando ya barabara inayoelekea shule ya Msingi ya Mavurunza mkono wa kushoto kutokea kituo cha mafuta Oryx Resort (Morogoro Road). Umbali kutoka barabarani ni mita 350.

 

HUDUMA YA KUTENGA KUNDI/ KANISA

Kanisa lilianza kama kundi la Kanisa la Chuo Kikuu tarehe 25 Mei, 1996 likiwa Mtaa wa Manzese chini ya uongozi wa Mchungaji Elienea Mnguruta. Na lilitengwa tarehe 04 Julai, 1999

 

Huduma ya kutenga Kanisa iliendeshwa na mtumishi wa Mungu Mchungaji Manento na jumla ya washiriki walioanzisha Kanisa walikuwa 99, na nguzo tatu za Kanisa zikiwa ni Exavery King’unge(Marehemu), Japhet Nyambega(Marehemu) na Mama Navoneiwa Kisaka.

 

UONGOZI WA KANISA

Baada ya kutengwa Kanisa uongozi wa kwanza uliochaguliwa kwa ngazi ya wazee ni kama ifuatavyo: Joshua Manyama, Abeid Kiangi na Jackson Biswaro(marehemu)

 

Kwa upande wa wachungaji wa mtaa kuanzia kutengwa Kanisa hadi hivi leo ni kama ifuatavyo:

Mch.  E. Mnguruta

Mch. S. Ngussa

Mch. M. Maliva

Mch. Gagi

Mch. R. Lukinga

Mch. Z. Mbuti Kusekwa na ndiye mchungaji mwanzilishi wa mtaa wa Kimara (2009-2013)

Mch. R. Mande(2013 mpaka tunapofikia hatua hii ya kuwekwa wakfu Kanisa)

 

UHAI WA KANISA (UINJILISTI)

Kanisa lilianza na idadi ya washiriki 99 hadi kufikia sasa idadi ya washiriki imeongezeka na kufikia 575 ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha Kanisa robo hii ya nne 2014.

 

Kanisa liliendelea kujishughulisha na kazi za uinjilisti katika Nyanja mbalimbali baada ya kutengwa mwaka 1999, ambapo hadi kufikia mwaka huu 2014 Kanisa limefanikiwa kutenga jumla ya makanisa manne yaliyokuwa Kanda/Makundi ya kanisa ambayo ni: Mbezi Luisi (ambapo kwa sasa ni makao makuu ya mtaa wa Mbezi), Kilungule, King’ongo na Suka. Pia Kanisa lilifanya uinjilisti katika maeneo mapya huko Kusini (Chiumbati - Mtwara) na kundi lilianzishwa na kujenga sehemu ya kuabudia, na hatimaye kundi hilo limekuwa Kanisa.

MAENDELEO YA KANISA

ENEO LA KANISA:    Kanisa linaeneo la kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 975 ambapo eneo lote lina mawe ya upimaji (Beacons).

 

JENGO LA KANISA:

Ujenzi wa jengo la Kanisa ulianza rasmi mwaka 1999. Na jengo hili lina sehemu kubwa mbili; Chini (Basement floor) ambapo kuna Kanisa la watoto na ofisi mbili. Kwa upande wa juu (Ground floor) kuna Kanisa la watu wazima, ofisi moja pamoja na chumba cha maandalio.

Pia, Kanisa limefanikiwa kujenga vyoo vya wanaume na wanawake vya kisasa, Kisima cha Ubatizo cha kisasa, pamoja na kujenga ghala la kutunzia vifaa vya Kanisa (store) na parking za magari.

 

Hadi tunafikia hatua ya kuweka Wakfu Kanisa 2014 makadirio ya gharama iliyotumika kwa ajili ya ujenzi ni jumla ya Tsh. 451,250,000/=

 

MWISHO

Taarifa hii imeandaliwa na ofisi ya Karani wa Kanisa mwaka 2014 kwa Kushirikiana na ofisi ya Wazee wa Kanisa.

                                           Hakimiliki © 2015, KimaraSdaChurch. Haki zote zimehifadhiwa