Seventh-Day Adventist Church

Kimara Sda Church Offical Website

Menu

Vijana wadogo

Add a Slideshow to see your custom images here
Chama cha vijana wadogo wa Kiadventista
Madhumuni ya chama ni kuwafundisha vijana wadogo uongozi na huduma ya Kikristo na kuwakuza wanachama hadi upeo wa uwezo wao.
Katika makanisa yenye shule, chama cha vijana wadogo ni sehemu ya mtaala na mwalimu mmoja ni kiongozi au mdhamini wa chama cha vijana wadogo. Chama cha vijana wadogo kinapoendeshwa katika shule, kila darasa huchukuliwa kama ni chama, na wanafunzi walio katika madarasa ya chini katika shule ya msingi huchukuliwa kama wanachama wanaoandaliwa. Wanafunzi wa madarasa ya juu ya shule ya msingi ni wanachama wa kawaida.
Kila mtu anayehusika na vijana lazima akidhi vigezo vya kanisa na vya kisheria, kama vile uchunguzi wa historia yake au kuwa cheti cha uthibitisho. Viongozi wa kanisa mahalia hawana budi kushauriana na konferensi ambayo itahakikisha na kushauri juu juu ya uchunguzi wa historia na vyeti vinavyoweza kupatikana na au kuhitajika.
                                           Hakimiliki © 2015, KimaraSdaChurch. Haki zote zimehifadhiwa