Seventh-Day Adventist Church

Kimara Sda Church Offical Website

Menu

Shule ya Sabato

Add a Slideshow to see your custom images here

Naetwe Manongi
Mkurugenzi- Idara ya Shule ya Sabato 2016

Shule ya Sabato ambayo ni programu ya msingi ya elimu katika kanisa, ina malengo manne: kusoma maandiko, ushirika, huduma kwa jamii na kusisitiza utume ulimwenguni. Idara ya shule ya Sabato na huduma binafsi ya Konferensi kuu husambaza miongozo ya kusoma Biblia kwa viwango vyote vya umri, hutoa miundo ya programu za shule ya Sabato katika muktadha wa utamaduni mbalimbali wa divisheni za ulimwenguni, hutoa miongozo na mifumo ya mafunzo kwa ajili ya walimu wa shule ya Sabato, na huhamasisha utoaji wa sadaka za shule ya Sabato kwa ajili ya utume wa ulimwengu.

"Shule ya Sabato ni tawi muhimu la kazi ya umisionari, siyo kwa sababu tu hutoa maarifa ya neno la Mungu kwa vijana na wazee, lakini kwa sababu huchochea ndani yao, moyo wa kuupenda ukweli mtakatifu wa neno hilo, na shauku ya kuusoma wao wenyewe; zaidi ya yote, huwafundisha kuendesha maisha yao kulingana na mafundisho matakatifu ya ukweli huo."- CSW 10,11.
"Shule ya Sabato, ikiendeshwa vizuri , ni moja kati ya zana kuu za Mungu kuwafanya watu wauelewe ukweli."- CSW 115
                                           Hakimiliki © 2015, KimaraSdaChurch. Haki zote zimehifadhiwa